Thursday, April 13, 2017

TUZO MCHEZAJI BORA: KANE, LUKAKU, IBRAHIMOVIC, SANCHEZ, HAZARD, KANTE WAGOMBEA, NANI KUIBUKA?

CHAMA CHA WACHEZAJI WA KULIPWA huko England PFA, Leo kimetoa orodha ya Wachezaji 6 ambao watagombea Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu huu.
6 hao ni Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic, Alexis Sanchez, Eden Hazard na N'Golo Kante.
Msimu uliopita Riyad Mahrez wa Leicester City alishinda Tuzo hii.
Kane na Lukaku pia wamo kwenye Listi ya Wgombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Vijana pamoja na Michael Keane, Leroy Sane, Jordan Pickford na Dele Alli ambae ni Mshindi wa Tuzo hii kwa Msimu uliopita.

Washindi wa Tuzo hizi 2 watatangazwa Aprili 23.
WAGOMBEA:
Tuzo Mchezaji Bora

Eden Hazard - Chelsea
Zlatan Ibrahimovic - Manchester United
Harry Kane - Tottenham Hotspur
N'Golo Kante - Chelsea
Romelu Lukaku - Everton
Alexis Sanchez - Arsenal 


Tuzo Mchezaji Bora Vijana
Dele Alli - Tottenham Hotspur
Harry Kane - Tottenham Hotspur
Michael Keane - Burnley
Romelu Lukaku - Everton
Jordan Pickford - Sunderland
Leroy Sane - Manchester City