Wednesday, April 12, 2017

UEFA EUROPA LIGI: KESHO ALHAMISI ANDERLECHT vs MAN UNITED, WAYNE ROONEY YUKO FITI

ALHAMISI Usiku moja ya Mechi za Robo Fainali za UEFA EUROPA LIGI ni ile itakayochezwa huko Brussels, Belgium kati ya Anderlecht na Manchester United.
Hiyo itakuwa ni mara ya 7 kwa Timu hizi kupambana na Rekodi yao ni Anderlecht Ushindi 2 Man Unite 3 na Sare 1.
Lakini moja kati ya Mechi hizo Man United iliifunga Anderlecht 10-1 kwenye Mechi ya Kombe la Ulaya iliyochezwa Tarehe 26 Septemba 1956 Uwanja wa Maine Road ambao ndio Uwanja wa zamani wa Man City Jijini Manchester.
Lakini Anderlecht ya sasa ni habari nyingine na imeshinda Mechi zao 5 kati ya 6 za Ulaya walizocheza mwisho Nyumbani kwao Msimu huu.

Nao Man United Msimu huu hawajafungwa Mechi yeyote ya Ulaya kati ya 6 walizocheza mwisho kwa Kushinda 5 Sare 1.
Lakini Rekodi ya Anderlecht kwa Klabu za England si nzuri kwani Wameshinda 7 Sare 5 Kufungwa 20 na katika Tripu zao 15 huko England wametoka Sare 2 na Kufungwa 13.
Mara ya mwisho kwa Man United kuivaa Klabu ya Belgium ni Msimu wa 2015/16 kwenye Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI walipoibwaga Club Brugge 7-1 katika Mechi 2 baada kuitwanga 4-0 huko Belgium.
Wakiwa na Bao 5 kila mmoja, Zlatan Ibrahimovic na Lukasz Teodorczyk wa Anderlecht wamebakia ndio Wafungaji wa Bao nyingi waliobakia kwenye Mashindano haya lakini wapo nyuma kwa Bao 3 kwa wanaoongoza ambao ni Mchezaji wa Zenit St Petersburg Giuliano na Edin Dzeko wa AS Roma. Licha ya Man United kusaka kutwaa Ubingwa wa Mashindano haya ili wafuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao, hili ndio Kombe pekee Ulaya ambalo hawajawahi kulitwaa.