Thursday, April 20, 2017

UEFA EUROPA LIGI: LEO MAN UNITED vs RSC ANDERLCHT

MECHI za Pili za Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Usiku Aprili 20 na Manchester United wako kwao Old Trafford wakihitaji ushindi au hata Sare ya 0-0 dhidi ya RSC Anderlecht ya Belgium ili kutinga Nusu Fainali.

Wiki iliyopita, Man United walitoka Sare 1-1 na Anderlecht huko Belgium na sasa wana matumaini makubwa ya kusonga kwani wana Rekodi nzuri Uwanjani kwao Old Trafford na pia dhidi ya Anderlecht ambayo waliwahi kuitandika 10-0 Mwaka 1956.

Mbali ya kuwa ni Kombe pekee la Ulaya ambalo Man United hawajawahi kulitwaa, kulibeba Kombe hili kutawafanya watinge moja kwa moja UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Mvuto mwingine kwa Wadau wa Soka wa Tanzania ni Mechi ya huko Ubelgiji kati ya KRC Genk na Celta Vigo ya Spain ambapo Mashabiki wengi Nchini wapo nyuma ya Nahodha wa Timu yetu ya Taifa, Mbwana Samatta, ambae ataongoza safu ya Fowadi ya KRC Genk wakisaka kupindua kichapo cha 3-2 walichopewa Wiki iliyopita.

REFA: Alberto Undiano Mallenco (Spain)
 

UEFA EUROPA LIGI
Tarehe Muhimu:

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI
24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden