Saturday, April 1, 2017

VPL FULL TIME: YANGA 1 vs 0 AZAM FC, MZAMBIA OBREY CHIRWA AIPANDISHA KILELENI YANGA!

VPL, LIGI KUU VODACOM, Leo imerudi kilingeni kwa Mabingwa Watetezi Yanga kuichapa Azam FC 1-0 kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kurudi kileleni mwa Ligi hiyo.
Bao la ushindi la Yanga lilifungwa Dakika ya 70 na Straika kutoka Zambia Obrey Chirwa.
Shangwe kwa Yanga kwa kupanda Kileleni
Ushindi huu umewafanya Yanga waongoze VPL wakiwa na Pointi 56 kwa Mechi 25 na Nafasi ya Pili ni Simba wenye Pointi 55 kwa Mechi 24.

Azam FC wanabaki Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 44 kwa Mechi 25.
Katika Mechi nyingine za hii Leo ya huko Mjini Mbeya, Mbeya City na Ruvu Shooting zilitoka Sare 1-1.
Jumapili zipo Mechi 4 na Macho Kodo ni huko Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kati ya Kagera Sugar, walio Nafasi ya 4, wakiwavaa Vinara Simba.
Nyingine za Jumapili ni Jijini Dar es Salaam kati ya African Lyon na Stand United, Mjini Mbeya ni Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar na huko Mwadui Complex, Shinyanga ni Mwadui FC na JKT Ruvu.

VIKOSI VILIVYOANZA:
YANGA:
Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Nadir Haroub, Vicent Bossou, Saidi Juma, Saimoni Msuva, Justine Zulu, Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke
Akiba: Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Andrew Chikupe, Juma Mahadhi, Geofrey Mwashiuya, Mateo Antony, Emanuel Martin

AZAM FC:
Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gradiel Michael, Yakubu Mohamed, Daniel Amoah, Himid Mao, Salumu Abubakar, Frank Domayo, Yahaya Mohamed, Shabaan Iddi, Ramadhan Singano
Akiba: Mwadini Ally, Abdalah Kheri, Bruce Kangwa, David Mwatika, Masoud Abdalah, Joseph Mahundi, Samuel Afful