Monday, April 10, 2017

FULL TIME VPL: MBAO FC 2 vs 3 SIMBA SC, MZAMIRU AFANYA MAAJABU CCM KIRUMBA LEO

Simba wanafunga bao la ushindi tena dakika za lala salama 3-2 dhidi ya Mbao Fc. Bao linafungwa na
Mzamiru kwa shuti kali na kufunga bao la tatu na la ushindi katika dakika hizo hizo 7 za nyongeza.Zikiwa zimeongezwa dakika 7 kumalizia dakika 90 Kipa wa Mbao Fc ya jijini Mwanza anafanya makosa tena kuruhusu mpira kudunda chini na mchezaji wa Simba kuumalizia langoni na kufanya bao kuwa 2-2.

Dakika ya 83 Simba wanapata bao na bao kuwa 2-1, Blagonon anaifungia Simba safi kwa kichwa baada ya kipa kutoka langoni mwake.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika Mbao Fc 2-0 Dhidi ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam. Simba kipindi cha pili wanatakiwa kuja kufanya mabadiliko na kuweza kupindua bao hizo mbili na kuweza kushinda mchezo huu kwani Mechi yao ya nyuma dhidi ya Kagera Sugar walichapwa bao 2-1 kwenye Dimba la Kaitaba Mjini Bukoba.Baadhi ya wachezaji wa Mbao Fc wakifurahia moja ya ushindi wao kwenye Ligi Kuu Vodacom Tanzania.Dakika ya 34 Mbao Fc wanapata bao la pili na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Simba Sc, Mfungaji ni Evarist
Mfungaji ni Geoge Sangija kipindi cha kwanza dakika ya 20.

Kipindi cha kwanza Timu ya Mbao Fc inapata bao la kungoza na kufanya 1-0 dhidi ya Simba Sc ya Jijini Dar es Salaam. Bao limefungwa dakika ya 19 kuelekea dakika ya 20 kipindi cha kwanza.Punde ni Mbao dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Taswira mchana huu Uwanja wa CCM Kirumba unavyoonekana