Saturday, April 22, 2017

ZLATAN IBRAHIMOVIC NA ROJO WATHIBITISHWA KUUMIA VIBAYA MAGOTI! KUKAA NJE MSIMU HUU WOTE 2016/17.

WACHEZAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na Marcos Rojo wamethibitika kuumia vibaya Magoti yao na wanatarajiwa kuwa nje kwa muda mrefu.
Wawili hao waliumia katika Mechi ya Alhamisi Usiku ambayo Man United waliifunga RSC Anderlecht 2-1 na kutinga Nusu Fainali ya UEFA EUROPA LIGI ambayo watacheza na Celta Vigo ya Spain.
Klabu ya Man United imethibitisha kuumia Magoti kwa Wawili hao lakini haikusema watakuwa nje kwa muda gani.
Ibrahimovic, ambae ndie Mfungaji Bora wa Man United Msimu huu akiwa na Bao 28, aliumia Goti lake baada kuurukia Mpira juu na kutua vibaya.
Rojo aliumia na kutolewa katika Dakika ya 23.
brahimovic, mwenye Miaka 35, alijiunga na Man United kama Mchezaji Huru mwanzoni mwa Msimu huu akitokea Paris St-Germain na kusaini Mkataba wa Mwaka Mmoja ambao sasa kulikuwa na mchakato wa kumuongezea Mwaka mwingine Mmoja.

Lakini kuumia kwa Rojo ndiko ambako kutaleta wasiwasi kwa Meneja Jose Mourinho kwani ana upungufu wa Masentahafu kwa vile Phil Jones na Chris Smalling nao ni Majeruhi.
Masentahafu waliobaki na ambao ni gfiti ni Eric Bailly na Daley Blind.

Mechi zinazofuata kwa Man United ni za Ugenini za EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya Burnley hapo Jumapili na Alhamisi ni huko Etihad dhidi ya Man City.Meneja wa Man United amesema kutokana na kuwakosa wachezaji hao, huduma zao ni muhimu sana na wenda Kikosi chake kikawa kwenye matatizo. Timu ya Machester ipo kwenye shida baada ya Wachezaji hao kuumia amesema Meneja Jose Mourinho. Kikosi kitakachoumana na Timu ya Burnley kitasukwa upya.