Tuesday, May 23, 2017

ANTONIO CONTE WA MABINGWA CHELSEA NDIE MENEJA BORA WA MSIMU – LMA!

MENEJA wa Mabingwa Wapya wa England Chelsea, Antonio Conte, ndie ameteuliwa kuwa Meneja Bora wa Msimu wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, na Chama cha Mameneja wa Ligi [League Managers Association].
Uteuzi huo wa Conte ulitangazwa Jumatatu Usiku kwenye Hafla ya 25 ya Chakula cha Usiku iliyofanyika huko London na kukabidhiwa Kombe ambalo sasa linaitwa SIR ALEX FERGUSON  TROPHY. 

 
Conte, akiwa kwenye Msimu wake wa kwanza tu na Chelsea, ambayo Msimu uliopita ilimaliza Nafasi ya 10 kwenye EPL, kutwaa Ubingwa wa England.
Msimu huu, Chelsea waliweka Rekodi ya kushinda Mechi 30 za EPL zikiwemo Mechi 13 mfululizo walizoshinda kuanzia Oktoba 1 na kumaliza Ligi wakiwa Mabingwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Tottenham.
Nae Chris Hughton ametwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka kwenye Daraja la Championship baada kuiwezesha Brighton kupanda Daraja na kutua EPL.
Kutoka Ligi 1, Meneja Bora ni Bosi wa Sheffield United Chris Wilder kwa kuisaidia Northampton kupanda Daraja na kuingia Championship.
Ligi 2, Meneja Bora ni Paul Cook baada kuiwezesha Portsmouth kutwaa Ubingwa wa Daraja hilo na kupanda.