Tuesday, May 30, 2017

ARSENE WENGER AKUBALI MKATABA MPYA WA MIAKA 2 ARSENAL!

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameafiki Mkataba Mpya wa Miaka Miwili wa kuendeleza himaya yake ya Miaka 21 Klabuni hapo.
FBL-ENG-FACUP-ARSENAL-CHELSEAJana Wenger na Mmiliki wa Hisa nyingi za Arsenal, Stan Kroenke, walikutana ili kuamua hatima yake na kuachia uamuzi wa mwisho kufanywa na Bodi ya Arsenal iliyoketi Leo Jijini London.
Klabu ya Arsenal imedokeza itatoa tamko rasmi Jumatano.
Mkataba wa Wenger hivi sasa unaishia Mwezi Juni.

Msimu huu uliokwisha Majuzi, Arsenal ilimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao ikiwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 20 tangu Wenger ajiunge Mwaka 1996.

FBL-ENG-FACUP-ARSENAL-CHELSEASasa, Arsenal, kwa Nafasi yao ya Ligi, ambayo pia kubeba FA CUP inawapa, Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI Hatua ya Makundi.https://pbs.twimg.com/media/DBExwlfXsAEf3KJ.jpg