Tuesday, May 2, 2017

ASFC: SIMBA NA MBAO KUKIPIGA JAMHURI DODOMA

Mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup - ASFC), kati ya Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, utafanyika Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”