Thursday, May 4, 2017

CRISTIANO RONALDO AZIDI KUTAMBA

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/14/1408026197922_wps_16_Cristiano_Ronaldo_of_Real.jpgCRISTIANO RONALDO ndie Mchezaji Bora Duniani.
Juzi Usiku ndani ya Estadio Santiago Bernabeu alionyesha tena umahiri wake alipopiga Hetitriki wakati Real Madrid ikiitandika Atletico Madrid 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hetitriki hiyo imeweka Rekodi na kumfanya Ronaldo awe Mchezaji wa Kwanza kufunga Hetitriki 2 mfululizo kwenye UCL.
Kwenye Raundi iliyopita, Ronaldo alifunga Bao 5 kati ya 6 wakati Real Madrid ikiitoa Bayern Munich ya Germany kwa Jumla ya Bao 6 katika Mechi 2.
Ronaldo pia ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, akiwa na Jumla ya Mabao 103.
PATA PICHA INAYOONYESHA NAMBA ZAKE: