Thursday, May 4, 2017

FIFA LISTI UBORA DUNIANI: BRAZIL BADO 1, ARGENTINA BADO 2, TANZANIA PALEPALE 135

https://vignette3.wikia.nocookie.net/logopedia/images/5/5c/FIFA_Logo.png/revision/latest?cb=20150211093210FIFA Leo imetoa Listi mpya ya Ubora Duniani kuibadili ile ya Mwezi iliyopita na hamna mabadiliko yoyote kwa zile zilizopo 20 Bora na pia Tanzania kubaki Nafasi yake ile ile ya 135.
Mwezi uliopita, Brazil ilikamata Nambari Wani Duniani na Tanzania kuchomoka kutoka Nafasi ya 157 iliyoshikilia Mwezi Machi na kupanda Nafasi 22 juu.
Nayo Brazil ilirejea kileleni kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 6 kwa kuitoa Argentina Namba 1.
Argentina sasa bado wapo Namba 2.
Egypt ndiyo Timu ya juu kabisa kwa Afrika ikishika Nafasi ya 19.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatoka Juni 1.