Wednesday, May 10, 2017

FIFA YACHUNGUZA UHAMISHO WA POGBA JUVENTUS KWENDA MAN UNITED

FIFA imesema inachunguza Uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United uliofanyika mwanzoni mwa Msimu huu.
Pogba, ambae mpaka sasa ameichezea Man United Mechi 48, aliuzwa na Juve kwa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 89.3.
FIFA imeiandikia Man United ikitaka taarifa za Uhamisho huo na hasa nani walihusika na Uhamisho na nini walilipwa.
Msemaji wa Man United ameeleza: "Hatuzungumzii Mikataba ya Watu. FIFA wana kila kitu tangu Uhamisho huo ufanyike Mwezi Agosti."
Hii ni mara ya pili kwa Pogba kuwepo Man United na alijiunga hapo kutoka Le Havre ya France Mwaka 2009 na kuuzwa kwa Juve Mwaka 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 1.5.

Alipouzwa na Juve kwenda Man United Mwezi Agosti ilisemwa zililipwa Euro Milioni 105 na pia Man United ilikubali kuilipa Juve Bonasi ya Euro Milioni 4.5 kutokana na mafanikio nabpia Euro Milioni 5 ikiwa Pogba atasaini Mkataba Mpyam
Upande wa Juve wao walisema wamevuna Euro Milioni 72.6 toka Uhamisho huo.