Monday, May 8, 2017

EPL: CHELSEA 3 vs 0 MIDDLESBROUGH, BLUES WANUKIWA NA UBINGWA! BORO WAWAFUATA SUNDERLAND KWA KUSHUKA DARAJA!

Vinara wa EPL Chelsea Ligi Kuu England, wakiwa kwao Stamford Bridge Jijini London wameitwanga Middlesbrough Bao 3-0 na kuishusha Daraja huku wao wakibakisha ushindi kwenye Mechi 1 tu ili watwae Ubingwa.
Sasa Chelsea wanaweza kuwa Mabingwa Ijumaa wakibakisha Mechi 2 ikiwa watashinda Ugenini huko The Hawthorns wakicheza na West Bromwich Albion.
Matokeo haya ya Leo yamewaunganisha Middlesbrough, maarufu kama Boro, pamoja na Sunderland kuteremshwa Daraja na sasa watacheza Daraja la chini ya EPL, la Championship, Msimu ujao.
Chelsea walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 23 kwa Pasi safi ya Cesc Fabregas na Diego Costa kukwamisha Mpira Wavuni.

Bao la Pili la Chelsea liliingia Dakika ya 34 Mfungaji akiwa Marcos Alonso aliemalizia Krosi ya Azpilicueta.
Hadi Haftaimu Chelsea walikuwa mbele kwa Bao 2-0.
Dakika ya 65 alikuwa tena Cesc Fabregas aliemsukia Nemanja Matic kupiga Bao la 3 na Chelsea kuongoza 3-0 Bao zilizodumu hadio mwisho.

VIKOSI:
CHELSEA:
Courtois, Azpilicueta, David Luiz [John Terry, 86’], Cahill, Moses, Fabregas, Matic, Alonso, Pedro [Chalobah 81'], Costa, Hazard [Willian, 72]
Akiba:
Begovic, Terry, Zouma, Ake, Chalobah, Loftus-Cheek, Willian.
MIDDLESBROUGH: Guzan, Fabio Da Silva, Chambers, Gibson, Friend, Clayton, De Roon, Forshaw [Leadbitter, 56], Traore [Bamford, 57'], Downing, Negredo [Gestede, 83']

Akiba: Konstantopoulos, Barragan, Bernardo, Leadbitter, Guedioura, Gestede, Bamford
REFA: Craig Pawson