Sunday, May 7, 2017

EPL..ARSENAL 2 vs 0 MANCHESTER UNITED, XHAKA NA WELBECK WAWEKA MATUMAINI KWA GUNNERS KUCHEZA UCL

Granit Xhaka celebrates with Nacho Monreal, Danny Welbeck and Kieran Gibbs after scoring the opening goalMechi s kati ya Arsenal na Man United iliyochezwa huko Emirate, Meneja wa Man United Jose Mourinho alibadili Kikosi chake Wachezaji 8 na pia kumtumia Chipukizi wa Miaka 19, Tuanzebe, aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Kikosi cha Kwanza huku pia ikimwingiza mpya mwingine McTominay kwenye Kipindi cha Pili.
Kabla ya Mechi hii, Jose Mourinho alidokeza kuweka mkazo kwenye UEFA EUROPA LIGI ambako Majuzi Alhamisi waliichapa Celta Vigo 1-0 huko Spain kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali na Alhamisi hii kurudiana huko Old Trafford.
Mshindi wa UEFA EUROPA LIGI hucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimi ujao.
Bao za Arsenal hii Leo zilifungwa Kipindi cha Pili Dakika za 54 na 57 na Granit Xhaka na Danny Welbeck.
Matokeo ya Leo yameiacha Chelsea ikiongoza Ligi ikiwa na Pointi 81 kwa Mechi 34 wakifuata Tottenham wenye Pointi 77 kwa Mechi 35, Liverpool ni wa 3 na wana Pointi 70 kwa Mechi 36, kisha Man City waliocheza Mechi 35 na wana Pointi 65.
Man United wamecheza Mechi 35 na wana Pointi 65 wakishika Nafasi ya 5 wakifuata Arsenal waliocheza Mechi 34 na wana Pointi 63.
Arsenal v Man Utd, EPL LIVE score: All the actionMtanange unaendelea mpaka sasa 18 bado ni 0-0Rooney na Welback waanza..
VIKOSI:
Arsenal XI:
Cech, Holding, Koscielny, Monreal, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka, Gibbs, Ozil, Alexis, Welbeck
Man United XI: De Gea, Tuanzebe, Smalling, Jones, Darmian, Carrick, Herrera, Mata, Rooney, Mkhitaryan, Martial