Tuesday, May 2, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: REAL MADRID vs ATLETICO MADRID

NUSU FAINALI ya Pili ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, itachezwa LEO Jumatano Usiku Stade Louis II, Monaco kati ya Wenyeji AS Monaco na Juventus ya Italy.
Mechi hii inakutanisha Difensi imara dhidi ya Washambuliaji hatari huku Monaco wakisifika kwa kupiga Bao nyingi wakati Juve wakifungwa Goli chache.
Monaco ni Timu yenye Vijana wengi wakati Juve ina Wakongwe na Wazoefu wengi.

Wakati Juve wakitumia Mfumo wa 4-2-3-1 chini ya Kocha Max Allegri ambao huhakikisha Pjanic, Dybala, Higuain, Mandzukic pamoja na Maveterani Buffon, Chiellini, Bonucci na Dani Alves wote kuwepo Uwanjani, Monaco, chini ya Kocha kutoka Ureno Leonardo Jardim, wao hung'ara kwa Mfumo wa kasi wa 4-4-2 unaotoa mwanya kwa Tineja wao wa Miaka 18 Kylian Mbappe kuliza Watu.
Tineja huyo, ambae amefunga Bao 18 katika Mechi 18 zilizopita, hupata sapoti kubwa toka kwa Almamy Toure, Bejamin Mendy, Bernardo Silva, na Nabil Dirar huku Radamel Falcao akiibuka upya Msimu huu na kupiga Bao 28.
Hii ni mara ya kwanza kwa Monaco kutinga Nusu Fainali tangu 2004 lakini mara 2 wamepigwa na Juventus kwenye Mashindano haya ya Ulaya.