Wednesday, May 31, 2017

MAN UNITED YAIWEKEA KIFUA REAL INAYOMTAKA KIPA DE GEA

Manchester United wanatarajia kuiwekea ngumu Real Madrid katika azma yao ya kumnasa Kipa wao David de Gea.
Mwaka 2015, Real Madrid, ambao Jumamosi wako huko Cardiff, Wales kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Juventus huku wakiwania kutetea Taji lao na kuwa Klabu ya Kwanza kufanya hivyo, walijaribu kumnunua De Gea lakini Dili ikakwama Dakika za mwisho katika Siku ya Mwisho ya Uhamisho huku pande zote zikiwa zimeafikiana Dau la Pauni Milioni 29.
De Gea, mwenye Miaka 26, alipigwa Benchi kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI hapo Mei 24 Man United wakiichapa Ajax 2-0 na kutwaa Kombe na langoni aliwekwa Kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina Sergio Romero.
Hivi sasa, kama ilivyo kawaida ya Spain, Magazeti ya huko hushabikia mno Klabu kubwa na yale ya upande wa Real Madrid kila kukicha hawakosa kupiga ‘mdogo mdogo’ kuhusu De Gea kutua kwa Mabingwa hao wa Spain.

Lakini hivi sasa, kupita ule Mwaka 2015 ambao De Gea alikuwa kwenye Mwaka wa Mwisho wa Mkataba wake, Kipa huyo mahiri ana Mkataba unaokwisha 2019 na hivyo Man United hawana presha kubwa.
Hadi sasa, habari toka ndani ya Klabu ya Man United, zimedokeza kuwa De Gea hajaomba Uhamisho kama ilivyo kwa Wachezaji ambao wana nia hiyo.
Image result for Manchester United