Tuesday, May 30, 2017

MICHAEL CARRICK KUBAKI OLD TRAFFORD MWAKA MWINGINE

KIUNGO wa Manchester United Michael Carrick amesaini Mkataba Mpya wa Mwaka Mmoja.
Carrick, mwenye Miaka 35, alitua Old Trafford kutoka Tottenham kwa dili ya £18.6m Mwaka 2006 na kucheza Mechi 458 akifunga Bao 24.
Carrick, ambae Mkataba wake wa sasa ulikuwa ukiisha Juni 4, ameeleza: "Nimefurahi safari yangu na hii Klabu Bora bado inaendelea!"
Hapo Juni 4 inatarajiwa kuchezwa Mechi Maalum Uwanjani Old Trafford kwa ajili ya kumuenzi Carrick kwa Utumishi wake mwema na Man United.
Meneja Jose Mourinho nae alizungumza: "Nimefurahi kufanya kazi na Michael Carrick Msimu huu wote. Mbali ya kuwa Mchezaji bora pia ni Binadamu mwema na mfano bora kwa Wachezaji Chipukizi!"
Carrick, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa England, akiwa na Man United ameweza kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI, EUROPA LIGI, FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.
Michael Carrick na Wayne Rooney ndio Wachezaji pekee toka England ambao wamefanikiwa kutwaa Makombe ya UEFA CHAMPIONS LIGI, EUROPA LIGI, FA CUP, Kombe la Ligi na Kombe la Dunia kwa Klabu.