Thursday, May 4, 2017

PENATI MFUMO MPYA 'ABBA' MBIONI KUANZA HIVI KARIBUNI!

UEFA ipo mbioni kufanya Majaribio Mfumo mpya wa Upigaji wa Mikwaju Mitano Mitano wa Penati ili kuondoa faida ya Timu inayoanza kupiga Penati hizo.
Utafiti uligundua Timu inayoanza kupiga Penati inayo Asilimia 60 ya nafasi ya kufuzu upigaji wa Penati hizo Tano Tano.
Mfumo huo Mpya, ambao unatambuliwa kama ABBA, utatumika kwa Timu ya Kwanza itayotambulika kama Timu A kupiga Penati ya Kwanza na kisha Timu B kupiga Penati ya Pili na ya Tatu na kisha Timu B kupiga Penati ya Nne halafu kuja zamu ya Timu A kupiga Penati ya 5 na ya 6 kwa kupokezana hivyo hivyo hadi kila moja inakamilisha Penati zake 5.
Mfumo huu umependekezwa na IFAB Chombo ambacho ndio pekee chenye Mamlaka ya kubadili Sheria za Soka.
Hivyo Mfumo wa sasa wa kupiga Penati moja moja kwa kila Timu kupokezana unaweza ukawa Historia ikiwa Majaribio ya Mfumo ABBA utafanikiwa.
UEFA imethibitisha ABBA itajaribiwa kwenye Mashindano ya EURO U-17 yaliyoanza Jana huko Croatia.
Kabla kupigwa kwa Penati kwa Mfumo wa ABBA Refa atarusha Shilingi Timu ipi itaanza kupiga na pia kupiga Kura kuamua Goli lipi la Uwanjani litatumika kupigiwa Penati hizo kama ilivyo sasa.
 

MFUMO ABBA:
-Penati ya Kwanza:
Timu A kutangulia
Timu B kufuatia
-Penati ya Pili:
Timu B kupiga mwanzo
Timu A kufuatia
-Penati ya 3:
Timu A kuanza
Timu B kufuatia
-Penati ya 4:
Timu B kuanza
Timu A kufuatia
-Penati ya 5:
Timu A kuanza
Timu B kufuatia