Friday, May 5, 2017

RATIBA LIGI KUU ENGLAND: CITY vs PALACE, LIVERPOOL vs SOUTHAMPTON, EMIRATES JUMAPILI ARSENAL vs MAN UNITED

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesisitiza hamna haja yeyote ya kusuluhishwa na Meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
Wawili hao wamekuwa na Historia ya mfarakano ndani na nje ya Uwanja na hata kufikia kutaka kuvaana Uwanjani wakati Mourinho yuko Chelsea.
Lakini kuelekea Mechi yao ya Jumapili ya EPL, Ligi Kuu England, Uwanjani Emirates, Mourinho, ambae hajawahi kufungwa na Wenger, amesisitiza hana tatizo na Wenger baada ya Jana Meneja huyo wa Arsenal kudai yeye yuko wazi kusitisha mfarakano na Mourinho.

JE WAJUA?
Uso kwa Uso - Ushindi:

Arsenal 81
Sare 47
Man United 96

Katika Mechi 10 zilizopita Arsenal imeshinda mara 2 na Man United ikishinda 4
Akiongea hii Leo, Mourinho amesema: “Hana haja ya kutaka suluhu kwa sababu hamna tatizo. Kukiwa na Amani sina tatizo.”
Aliongeza: “Mara ya mwisho tulipocheza Old Trafford tulipeana mikono kabla na baada ya Mechi. Mie nipo kwenye Soka Maisha yangu yote. Kama kuna tatizo Uwanjani, Siku ya Pili si tatizo tena!”
Kisha Mourinho, kama kawaida, akapiga kijembe: “Sina tatizo, nadhani atafurahi kuhusu mimi nikibadili Timu itayocheza na Arsenal. Nadhani atanifurahia sana mimi!”

EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:

Ijumaa Mei 5
2200 West Ham United v Tottenham Hotspur

Jumamosi Mei 6
1430 Manchester City v Crystal Palace
1700 Bournemouth v Stoke City
1700 Burnley v West Bromwich Albion
1700 Hull City v Sunderland
1700 Leicester City v Watford
1930 Swansea City v Everton

Jumapili Mei 7echi 35

15:30 Liverpool v Southampton
18:00 Arsenal v Manchester United

Jumatatu Mei 8
2200 Chelsea v Middlesbrough