Sunday, May 28, 2017

SIMBA SASA WA KIMATAIFA, WAIBWAGA MBAO FC 2-1, KUCHEZA AFRIKA!


SIMBA, Leo huko Jamhuri Stadium, Dodoma, wamekuwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup - ASFC) baada ya kuifunga Mbao FC 2-1 katika Fainali iliyokwenda Dakika 120.

Timu hizi zilikuwa 0-0 hadi Dakika 90 na Gemu kulazimika kuongezwa Dakika za Nyongeza 30 na ndipo Bao zote kupatikana.

Bao la kwanza la Simba lilifungwa Dakika ya 95 Mfungaji akiwa Blagnon na Mbao kusawazisha kwa Goli la Robert Ndaki la Dakika ya 109.

Lakini, Dakika ya mwisho, ya 120, Refa Ahmad Kikumbo akawapa Penati Simba ambayo Wadau wengi wanadai ni tata na Kichuya kuipa Simba Bao la Pili na la ushindi.

Simba sasa wataiwakilisha Nchi kwenye Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Msimu ujao ikiwa ni mara yao ya kwanza tangu 2013.

Ushindi huu wa Leo na kurudi kucheza Michuano ya Kimataifa ni faraja kubwa kwa Simba kwani mapema Leo kuliibuka stori kuwa FIFA wameipiga chini Simba kwa kuikataa Rufaa yao iliyokuwa ikidai Pointi 3 kwenye VPL, LIGI KUU VODACOM, ambazo walipokwa, na ambazo kama wangezipata wangepewa Ubingwa wa Ligi hiyo ambayo Mabingwa wake ni Yanga.