Saturday, May 27, 2017

UHAMISHO 2017: BERNARDO SILVA ATUA CITY

Manchester City's new signing Bernardo SilvaBernardo Silva Kiungo wa AS Monaco anaetoka Portugal,  Amekamilisha Dili ya kutua Manchester City kwa kitita cha Pauni Milioni 43.
Msimu huu, Silva, mwenye Miaka 22, aliisaidia sana Monaco kutwaa Ubingwa wa Ligi 1 huko France na pia kuifikisha Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Silva ameichezea Timu ya Taifa ya Portugal mara 12 na kufunga Bao 1 na kukipiga Mechi 58 na Monaco akifunga Bao 11.