Sunday, May 7, 2017

YANGA YAIPIGA 2-0 PRISONS NA KUKAA KILELENI, JKT RUVU YASHUSHWA DARAJA!!

Kikosi cha JKT Ruvu

MABINGWA WATETEZI YANGA Leo wamerudi kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom, baada kuichapa 2-0 Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao za Yanga zilifungwa na Amissi Joselyn Tambwe Dakika 71 na Obrey Chirwa Dakika ya 75.
Ushindi huu umewafanya Yanga kuwa na Pointi 59 kwa Mechi 26 sasa wan a Simba ambao wamecheza Mechi 1 zaidi lakini wamezidiwa kwa Ubora wa Magoli.
Huko CCM Kirumba Mwanza, Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1 na kuishusha Daraja.
VIKOSI:
YANGA:
Benno Kakolanya, Hassan Kessy [Juma Abdul 59], Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’ [Haruna Niyonzima 65], Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa [Matheo Anthony 81], Geoffrey Mwashiuya

TANZANIA PRISONS:

 Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Michael Ismail, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya, Mohammed Samatta [Nchinjay Kazungu 86], Victor Hangaya [Kassim Hamisi 63], Lambert Sibiyanka, Meshack Suleiman
REFA: Suleiman Kinugani [Morogoro]
Msimamo kwa Hisani ya 'Naipenda Yanga"

VPL – LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Mei 6
Yanga 2 Tanzania Prisons 0
Toto African 2 JKT Ruvu 1
Ruvu Shooting 1 Kagera Sugar 1
Maji Maji FC 3 Mwadui FC 0
Azam FC v Mbao

Jumapili Mei 7
Simba v African Lyon