Saturday, May 27, 2017

ZABALETA HUYOO WEST HAM UNITED

West Ham Wamemsaini Beki Pablo Zabaleta kama Mchezaji Huru kutoka Manchester City mara tu baada ya Mchezaji huyo kutoka Argentina kumalizika Julai 1.

Zabaleta aliagwa rasmi na Man City Mei 17 baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Miaka 9 akiwa Mchezaji wa 3 kudumu kwa Miaka mingi akiwafuata Joe Hart na Vincent Kompany.

Zabaleta, mwenye Miaka 32, alijiunga na City kutoka Espanyol ya Spain Mwaka 2008 kwa Dau la Pauni Milioni 6.5 na kuichezea Klabu hiyo Mechi 333 akitwaa Ubingwa wa England mara 2, Kombe la Ligi mara 2 na FA CUP.