Thursday, June 22, 2017

BAYERN YAZIONYA CHELSEA NA MAN UNITED JUU YA ROBERT LEWANDOWSKI

Image result for Robert LewandowskiBayern Munich imeziambia Chelsea na Manchester United kusahau kabisa kumsaini Robert Lewandowski kipindi hiki cha Uhamisho. Image result for Robert LewandowskiBayern Munich imesisitiza hamna nafasi hata chembe kwa Lewandowski kuihama Klabu hiyo ya Germany hivi sasa.
Hivi karibuni Wakala wa Lewandowskit, Maik Barthel, alitoboa kuwa Staa huyo wa Poland hakuwa na furaha na Bosi wa Bayern Carlo Anceloti na Wachezaji wenzake kwa kushindwa kumsaidia kutwaa Buti ya Dhahabu ya Bundesliga anayopewa Mfungaji Bora wa Ligi hiyo.
Buti hiyo ilitwaliwa na Straika wa Borussia Dortmund anaetoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliepachika Bao 31 huku Lewandowski akifunga Bao 30.

Maik Barthel aliliambia Gazeti la Germany Kicker: "Robert aliniambia hakupata sapoti ya na Kocha hakuamrisha asaidiwe ili afunge Bao zaidi awe Mfungaji Bora. Hilo lilimvunja moyo sana!”

Matamshi hayo yakaibua hisia kuwa Lewandowski atahama na Klabu za England Chelsea na Man United kumkodolea macho na kuhusishwa sana na kumchukua Straika huyo mwenye Miaka 28.

Lewandowski, ambae amewafungia Mabingwa hao wa Germany Mabao 110 katika Misimu Mitatu, alisaini Mkataba Mpya na Bayern Mwezi Desemba 2016 ambao utamweka kwa Miaka Mitatu zaidi.
Kufuatia hali hii ya utata Klabu ya Bayern imetoa tamko kali: “Bayern Munich haipotezi muda kuhusu Uhamisho wa Lewandowski. Hamna mazungumzo na Klabu yeyote na hayatakuwepo. Ikiwa Klabu nyingine zinataka kuzungumza na Wachezaji, wenye Mikataba ya muda mrefu, wapo hatarini kuadhibiwa na FIFA. Hata Wakala wake ametuhakikishia hakuna mazungumzo ya Uhamisho yanayofanyika.”