Sunday, June 4, 2017

FULL TIME..CARRICK'S TESTIMONIAL: UNITED '08 2 vs 2 ALL-STARS, MICHAEL CARRICK AISAWAZISHIA BAO NA KUUMALIZA KWA SARE

Michael Carrick testimonial LIVE: Old Trafford updates
KWENYE Mechi yake mwenyewe kumuenzi kwa Utumishi wako ulitukuka kwa Manchester United, Michael Carrick alifunga Bao safi la Mita 25 la Dakika ya 82 na kuwapa Sare ya 2-2 Kombaini ya Man United walipocheza na Mastaa Wateule wa Michael Carrick.

Mechi hii ilichezwa Leo Uwanjani Old Trafford Jijini Manchester na kuhudhuriwa na Watazamaji 70,027,
Mapato ya Mechi hii yatakwenda kwenye Mifuko ya Hisani kusaidia Watoto na Vijana.
Mara mbili, Man United, iliyosimamiwa na Sir Alex Ferguson akiongoza Wchezaji wengi waliotwaa Ubingwa wa England na ule wa Ulaya Mwaka 2008, ilitoka nyuma na kusawazisha.

Gaizka Mendieta aliwapa Kikosi cha Nyota wa Carrick uongozi Dakika ya 22 na Nemanja Vidic kusawazisha kwa Kichwa.
Lakini Nyota hao, waliokuwa chini ya Meneja Harry Redknapp, walikwenda tena mbele na kuongoza 2-1 kwa Bao la Dakika ya 64 la Robbie Keane.
Ndipo mwenyewe Michael Carrick alipowasha kigongo cha Mita 25 na kuwapa Sare ya 2-2 Man United 08.

Michael Carrick testimonial LIVE: Old Trafford updates
Carrick's testimonial LIVE:HALF-TIME: UNITED '08 1-1 ALL-STARShttp://i.dailymail.co.uk/i/pix/2017/06/04/14/1496584074012_lc_galleryImage_Britain_Football_Soccer_M.JPG
THE SQUADS
Manchester United '08 XI:
Edwin van der Sar, Gary Neville, Wes Brown, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Mikael Silvestre, Patrice Evra, Michael Carrick, Paul Scholes, Ryan Giggs, Ji-sung Park, Owen Hargreaves, Anderson (injured), Darren Fletcher, Wayne Rooney, Louis Saha, Dimitar Berbatov.

Michael Carrick All-Stars: Shay Given, Phil Neville, Michel Salgado, Jamie Carragher, John Terry, Eric Abidal, Joan Capdevila, Steven Gerrard (injured), Frank Lampard (injured), Marcos Senna, Gaizka Mendieta, Clarence Seedorf, Damien Duff, Richard Garcia, Michael Owen, Robbie Keane, Eidur Gudjohnsen.