Friday, June 16, 2017

CHELSEA WAPINGA TAARIFA ZA ANTONIO CONTE KUTAKA KUODOKA

KLABU ya Chelsea imesisitiza Meneja wao Antonio Conte anafurahia kuwepo hapo licha kuzagaa kwa ripoti kuwa anataka kuondoka.
Conte aliripotiwa kuchukizwa na utawala wa Chelsea kwa kushindwa kujikita kwenye Soko la Uhamisho wa Wachezaji ambao yeye aliwataka ili kuimarisha Kikosi chake kwa ajili ya Kampeni ya Mashindano ya Ulaya ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Lakini Chelsea, kupitia Sky Sports News HQ Jijini London, inaamini Conte, ambae sasa yupo Vakesheni, atarejea mwanzoni mwa Julai kuitayarisha Timu kwa ajili ya Msimu Mpya.
Conte, katika Msimu wake wa kwanza tu na Chelsea, aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, na amebakiza Miaka Miwili katika Mkataba wake na Chelsea.

Mara baada ya kutwaa Ubingwa, Conte alisikika akisema anataka kubakia Chelsea kwa muda mrefu lakini akakiri kwa Soka la sasa hilo ni gumu.

Hivi karibuni Straika wa Chelsea Diego Costa alidai Conte alimtumia ujumbe wa simu kwamba hahitajiki kwa Msimu ujao na jambo hilo huenda likawa limezua msuguano kati ya Conte na uongozi wa Chelsea.

Kwani kwa kupasua kuwa Costa anauzwa Chelsea inaona thamani ya kuuzwa kwa Conte itaporomoka.

Lakini inaaminika Conte tayari ashawapa Wakurugenzi wa Ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo na Marina Granovskaia, Listi yake ya Wachezaji anaetaka waletwe Stamford Bridge.