Thursday, June 15, 2017

CLAUDE PUEL ATIMULIWA SOUTHAMPTON, NANI KUCHUKUWA NAFASI YAKE

Claude Puel ametimuliwa kama Meneja wa Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’ baada ya kudumu Msimu Mmoja tu.
Puel, Raia wa France mwenye Miaka 55, aliteuliwa kuwa Meneja Juni 2016 na Msimu uliopita aliikita Southampton Nafasi ya 8 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, ikipoteza Mechi 16.

Pia aliifikisha Fainali ya EFL CUP Februari, ikiwa ndio Fainali yao ya kwanza tangu 2003, na kuchapwa 3-2 na Manchester United.
Klabu ya Southampton imethibitisha kutimuliwa kwa Puel na sasa imesema inasaka Meneja Mpya.

Puel, alietokea Nice ya France ambako alikaa Miaka Minne, alimrithi Ronald Koeman hapo Southampton.
Puel anakuwa Meneja wa 3 kutimka Southampton katika Miaka Mitatu iliyopita baada ya Mauricio Pochettini kwenda Tottenham na Koeman kutimkia Everton.