Sunday, June 25, 2017

COSAFA CUP: TANZANIA 2 vs 0 MALAWI

lesmal6Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeanza vyema  kampeni za kucheza hatua ya Robo fainali kwa kucheza na Malawi leo hii Jumapili, Juni 25 dhidi ya timu ya malawi, michezo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa).
B16GZMN0153Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa katika mashindano hayo na imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Kinara wa kila kundi atakwenda moja kwa moja hatua ya robo fainali.