Friday, June 16, 2017

CRISTIANO RONALDO ATAKA UONDOKA SPAIN

b1Cristiano Ronaldo amewaambia Real Madrid anataka kuondoka Real Madrid Dirisha hili la Uhamisho.
Imeripotiwa kuwa Supastaa huyo kutoka Ureno amempasha Rais wa Real, Florentino Perez, anataka kuondoka Spain mara tu baada ya kuburuzwa Mahakamani akishitakiwa kwa Ukwepaji Kulipa Kodi.
Ronaldo ameshitakiwa Mahakamani kwa kukwepa kulipa Kodi ya Spain ya Euro Milioni 14.7 kitu ambacho amepinga vikali.

Kwa mujibu wa Gazeti la Ureno A Bola, Ronaldo mwenye Miaka 32, amekasirishwa mno na jinsi alivyotendewa na sasa anataka kuihama Nchi ya Spain.
Hadi sasa Klabu ya Real haijatamka lolote kuhusun ripoti hizi lakini ni wazi Rais Perez hatataka Mchezaji Bora Duniani ambae amewabebesha Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu huu uliokwisha hivi karibuni ang’oke hapo.
Ronaldo, ambae ametwaa Ballon d’Or mara 4, ameifungia Real Mabao 406 katika Mechi zake 394 tangu atue hapo kutoka Manchester United Mwaka 2009.
Akiwa na Real amevunja Rekodi kadhaa na kutwaa Mataji makubwa yakiwemo UEFA CHAMPIONS LIGI 3, La Liga 2 na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu 2.

Hivi sasa Ronaldo ana Mkataba na Real hadi 2021 na Uhamisho wowote utakaomhusu yeye ni lazima utakuwa wa Dau la Rekodi ya Dunia.