Monday, June 5, 2017

EDEN HAZARD: KIUNGO WA CHELSEA AVUNJIKA ENKA MAZOEZINI NA TAIFA BELGIUM, NJE WIKI 7 MPAKA 8

http://ichef.bbci.co.uk/onesport/cps/800/cpsprodpb/59AA/production/_96345922_gettyimages-543169630.jpgKIUNGO wa Mabingwa wa England Chelsea, Eden Hazard, amevunjika Enka yake ya Mguu wa Kulia akiwa Mazoezini na Timu ya Taifa ya Belgium kwa mujibu wa Taarifa za Chama cha Soka cha Belgium, RBFA.
Awali RBFA ilitoa Posti ya Twitter ikisema Mchezaji huyo aliteguka Enka na baadae kutolewa nyingine ikithibitisha kuvunjika Enka ya Kulia baada uchunguzi wa kina.

Hazard, mwenye Miaka 26, sasa ataikosa Mechi ya Kirafiki kati ya Belgium na Czech Republic itayochezwa Leo usiku na pia ile Mechi ya Kundi lao la Nchi za Ulaya kuwania Nafasi za Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia Mwaka 2018.

Hazard aliisaidia sana Chelsea kutwaa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, akifunga Bao 16 katika Mechi 36 alizocheza.

Bado Mchezaji huyu ana Mkataba wa Miaka Mitatu na Chelsea lakini hivi karibuni upo uvumi mkubwa kuhusishwa na kuhamia kwa Mabingwa wa Spain na Ulaya Real Madrid.

Chelsea confirm Eden Hazard will be out for three monthsHadi sasa haijajulikana atakuwa nje kwa muda gani lakini inadaiwa si chini ya Wiki 8 na hilo litamfanya awezi kuikosa Mechi ya Kufungua Pazia Msimu Mpya wa 2017/18 huko England ambayo Mabingwa Chelsea watacheza na Mabingwa wa FA CUP, Arsenal, itakayochezwa Wembley Jijini London hapo Jumapili Agosti 6.

EPL itaanza rasmi Agosti 12.