Tuesday, June 20, 2017

JOSE MOURINHO ABURUZWA KWA PILATO KWA MADAI YA UKWEPAJI KODI

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho nae ameungana na mlolongo wa Mastaa Wachezaji Soka walioburuzwa Mahakamani huko Nchini Spain kwa tuhuma za Ukwepaji Kulipa Kodi.
Imedaiwa Mourinho amekwepa kulipa Kodi ya kiasi cha Pauni Milioni 2.9, Euro Milioni 3.3, aliyopaswa kulipa kati ya Miaka 2011 na 2012.

Mwendesha Mashitaka kwenye Mahakama ya Spain amedai Mourinho hakubainisha Mapato yake yatokanayo na Mauzo ya Umiliki wake wa Picha na Matangazo mengine.

Mashitaka ya Mourinho, mwenye miaka 54, ni Mawili ya kukwepa Kodi ya Euro Milioni 1.6 Mwaka 2011 na Euro Milioni 1.7 Mwaka 2012.
Mourinho mwenyewe hajatamka lolote kuhusu tuhuma hizi.
Mastaa wengine wa Soka walioandamwa na Kesi za aina hii ni pamoja na Cristiano Ronaldo anmbae Wiki iliyopita alifunguliwa rasmi Mashitaka kiasi cha kumuudhi na sasa ametishia kuihama Spain na kuacha kuichezea Real Madrid.

Wengine waliowahi kushitakiwa na kuhukumiwa ni Fowadi wa Barcelona, Lionel Messi, ambae alipigwa Faini na kuamriwa ende Jela Miezi 21 ingawa Kifungo hiki kinaaminika kitakuwa cha nje, na Javier Mascherano wa Barcelona aliefungwa Kifungo cha nje cha Mwaka Mmoja.