Wednesday, June 14, 2017

LIGI KUU ENGLAND MSIMU MPYA 2017/18: RATIBA HADHARANI, MABINGWA CHELSEA VS BURNL2EY, ARSENAL VS LEICESTER CITY, MAN UNITED VS WEST HAM UNITED

MABINGWA Chelsea wataanza Msimu Mpya wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, wa 2017/18 utakaoanza Wikiendi Agosti 12 kwa kucheza Nyumbani na Burnley.
Mechi ya Pili kwa Chelsea ni Ugenini huko Wembley kuivaa Tottenham ambao walimaliza EPL Nafasi ya Pili.
Arsenal wataanza kwao Emirates kucheza na Mabingwa wa zamani Leicester City lakini Agosti 26 wako huko Anfield kuivaa Liverpool.
Man United wataanzia kwao Old Trafford dhidi ya West Ham wakati Man City wapo Ugenini kucheza na Timu Mpya iliyopanda Daraja Brighton.
Wapya wengine, Mabingwa wa Daraja la Championship, Newcastle, wapo kwao St James' Park kucheza na Tottenham.

MECHI ZA UFUNGUZI - WIKIENDI YA AGOSTI 12:
Arsenal v Leicester City
Brighton and Hove Albion v Manchester City
Chelsea v Burnley
Crystal Palace v Huddersfield Town
Everton v Stoke City
Manchester United v West Ham United
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Southampton v Swansea City
Watford v Liverpool
West Bromwich Albion v Bournemouth