Saturday, June 3, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE, JUVENTUS 1 vs 4 REAL MADRID, REAL WATETEA UBINGWA WAO, CRISTINO RONALDO AWEKA REKODI!


MABINGWA WATETEZI Real Madrid Leo wamekuwa Timu ya Kwanza kumudu kutetea Ubingwa wao baada ya kuitandika Juventus Bao 4-1 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyochezwa huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales.
Hii ni mara ya 12 kwa Real Madrid kuwa Mabingwa wa Ulaya.
Kwa Juventus, ambao wameshinda Fainali zao 2 tu kati ya 8 walizotinga, sasa wamefungwa katika zote 5 walizofika mara ya mwisho ambazo ni za Miaka ya 1997, 1998, 2003, 2015 na hii ya Leo.
Tangu AC Milan wafanikiwe kutetea Ubingwa wa Ulaya Miaka ya 1989 na 1990, wakati huo Kombe hili likiitwa, EUROPAEN CUP, hakuna Timu iliyowahi kutetea Taji hili la UEFA CHAMPIONS LIGI hadi hii Leo Real Madrid kuweka Historia hii.
Kwa Mchezaji Bora Duniani sasa amefikisha Maba 105 ya UCL na Msimu hu undie Mfungaji Bora wa Mashindano haya akiwa na Bao 12 akimpiku Lionel Messi wa Barcelona aliefunga Bao 11.

MAGOLI:
Juventus 1

Mario Mandzukic 27

Real Madrid 4
Cristiano Ronaldo 20
Carlos Casemiro 61
Cristiano Ronaldo 64
Marco Asensio 90

Juve walimaliza Fainali hii wakibaki Mtu 10 baada ya Juan Cuadrado, alieingizwa Uwanjani Kipindi cha Pili, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.

VIKOSI:
Juventus:
Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Alves, Sandro, Pjanic, Khedira, Dybala, Mandzukic, Higuain.
Akiba:Neto, Benatia, Lichsteiner, Cuadrado, Marchisio, Lemina, Asamoah

Real Madrid:Navas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Casemiro, Modric, Isco, Kroos, Benzema, Ronaldo.
Akiba:Casilla, Nacho, Bale, Kovacic, Asensio, Morata, Danilo
REFA:Felix Brych (Germany)
Real Madrid vs Juventus, UEFA Champions League final LIVEhttp://i1.mirror.co.uk/incoming/article10554535.ece/ALTERNATES/s1176b/BANNER-Juve-Goal.jpg