Tuesday, June 6, 2017

LUKAKU KUTUA CHELSEA, JUVE AU MAN UNITED?

Romelu Lukaku amekiambia Kituo cha TV cha Sky Sports kwamba tayari anajua Msimu Mpya wa 2017/18 unaoanza Agosti 12 atachezea Klabu ipi.
Straika huyo wa Everton hajasaini Mkataba Mpya huku akihusishwa kuhama na Klabu za Chelsea, Juventus na Manchester United zinatajwa sana kumtaka.
Lukaku, mwenye Miaka 24, amekuwa msiri mno na azma yake lakini Jana mara baada kuichezea Nchi yake Kirafiki Belgium na Czech Republic na kuifunga Bao 2-1, alieleza kuwa uamuzi umeshafikiwa.
lukaku-chelsea.jpg
Amesema: "Wakala wangu anajua nini kitatokea. Mimi najua nataka kufanya nini na chochote kikitokea nyie mtaambiwa!"
Huko Everton, Lukaku nusura asaini Mkataba Mpya Mwezi Machi lakini akasita na kudai nia yake ni kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Msimu uliopita, ulioisha Mwezi uliopita, Lukaku alipiga Bao 25 wakati Everton ikimaliza Nafasi ya 7 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Ijumaa Lukaku atakuwa tena Uwanjani kuichezea Belgium ikipambana Ugenini na Estonia kwenye Mechi ya Kundi H la Nchi za Ulaya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Kwenye Kundi hilo, Belgium wako juu na wana Pointi 13 wakifuata Greece 11, Bosnia and Herzegovina 10, Cyprus na Estonia wana 4 kila mmoja na mkiani ni Gibraltar 0.
Mechi za Kundi H ni Ijumaa Juni 9 ambazo ni Bosnia And Herzegovina v Greece, Estonia v Belgium na ile ya Gibraltar v Cyprus.