Monday, June 26, 2017

MAN CITY NA ARSENAL KWENYE MAZUNGUMZO YA SANCHEZ NA AGUERO

Arsenal na Manchester City zimeripotiwa zipo kwenye mazungumzo mazito ya kubadilishana Mastraika wao Alexis Sanchez na Sergio Aguero katika Kipindi hiki cha Uhamisho kinachoanza Julai Mosi.
Mastraika hao Wawili wote wamehusishwa na kuhama Klabu zao hivi sasa lakini hakuna mmoja aliepata Klabu thabiti.
Imeripotiwa Meneja wa Man City Pep Guardiola amekuwa akimtaka Alexis Sanchez lakini Arsenal wamekuwa wagumu kumtoa Mchezaji yao kwa Wapinzani wao wa EPL, Ligi Kuu England.
Hata hivyo, ripoti hizi zimetoboa kuwa Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, atakuwa tayari kumtoa Sanchez kwa kubadilishana na Aguero wa City.
Arsenal wanaweza kuiendeleza Dili hii hasa kwa sababu wamekwama katika azma yao ya kumnunua Alexandre Lacazette wa Lyon ya France baada ya Klabu zote kushindwa kuafikiana Dau la Uhamisho.
Lyon wamekuwa wakitaka walipwe Dau la Pauni Milioni 57 lakini Arsenal ni wagumu wa kutoa kiasi hicho cha Fedha.