Tuesday, June 27, 2017

MAN UNITED WAKARIBIA KUMSAINI KIUNGO WA CHELSEA NEMANJA MATIC

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2016/06/ma1-1500x1000.jpg?w=960&strip=allMwenyewe Matic ameripotiwa kutaka sana kuungana na Meneja wa Man United Jose Mourinho ambae ndie alimrudisha tena Matic kutoka Benfica ya Ureno Mwaka 2014.
Man United wamekuwa wakiongea na Chelsea kuhusu Uhamisho huu unaomhusu Matic mwenye Miaka 28 na inaaminika Dili ya Dau linalokaribia Pauni Milioni 40 inakaribia kukamilika.

Msimu uliopita, Matic alikuwa sehemu muhimu ya Kikosi cha Meneja Antonio Conte kilichopeleka Ubingwa huko Chelsea akicheza Mechi 35 za EPL, LIGI KUU ENGLAND, kati ya 38.
Kuondoka kwa Matic kumesaidiwa hasa na Chelsea kukaribia kumsaini Kiungo kutoka AS Monaco Tiemoue Bakayoko na hilo limemfanya Conte abariki Uhamisho wa Matic.

Kwa Mourinho, kutua kwa Matic ni nafasi murua kupata Mrithi wa muda mrefu wa Kiungo Michael Carrick, ambae nae ameongezewa Mkataba wa Mwaka Mmoja, lakini pia ni kutoa mwanya kwa Paul Pogba kuwa Kiungo Mshambuliaji halisi.

Ikiwa Dili hii itakamilika, basi Matic atakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Man United katika Kipindi hiki baada ya kumsaini Victor Lindelof kutoka Benfica kwa Dau la Pauni Milioni 30.