Tuesday, June 20, 2017

MBEYA CITY YAANZA KUSAJILI, YAMSAJILI BEKI ERICK KYARUZI MOPA

Mchezaji huyo hakumaliza msimu uliopita baada ya kusimamishwa na uongozi wa Kagera kwa tuhuma za kuihujumu ilipocheza dhidi ya Yanga.
Dar es Salaam. Klabu ya Mbeya City imeanza usajili kwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu beki wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi Mopa.
Mchezaji huyo hakumaliza msimu uliopita baada ya kusimamishwa na uongozi wa Kagera kwa tuhuma za kuihujumu ilipocheza dhidi ya Yanga.
Akizungumza na mtandao MCL Digital, Kyaruzi amesema anafurahi kuanza maisha mapya na Mbeya City msimu ujao.

"Nilikuwa na wakati mgumu kama mchezaji, lakini nashukuru nimeanza mwanzo mpya. Nimesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na ninaamini nitatoa mchango mkubwa katika timu,"alisema Kyaruzi.
Aliongeza kuwa amedhamiria kurejesha uwezo wake msimu ujao akiwa na timu yake mpya.
Kyaruzi anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mbeya City tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Juni 15.