Monday, June 12, 2017

MORATA ATAREJEA REAL AU SAFARI OLD TRAFFORD?

Nahodha wa Real Madrid Mabingwa wa Spain na Ulaya, Sergio Ramos, amekiri hajui kama Mchezaji mwanzake Alvaro Morata atarejea Madrid huku akivumishwa kutinga England kujiunga na Manchester United.
Morata anadaiwa kutaka kucheza mara kwa mara baada kuanza Mechi 14 tu za La Liga wakati Real ikibeba Ubingwa wa Ligi hiyo pamoja na UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ulioisha Mwezi Mei.
Morata, mwenye Miaka 24, pia ni Mchezaji wa Kimataifa wa Spain na Msimu uliopita aliifungia Real Bao 20.
Akiulizwa na Wanahabari mara baada ya Jana Spain kuichapa Macedonia 2-1 huko Skopje katika Mechi ya Kundi G la Nchi za Ulaya kuwania kucheza Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018, Ramos alijibu: "Tutajua kama ataondoka au la. Si mie ninaeamua!"