Tuesday, June 20, 2017

NEMANJA MATIC WA CHELSEA ATAKA KUJUMUIKA TENA NA MOURINHO PALE OLD TRAFFORD

RIPOTI nzito zimetokea kuwa Staa wa Chelsea Nemanja Matic anataka kujumuika tana na Jose Mourinho huko Manchester United.
Mourinho ndie aliempeleka Matic huko Stamford Bridge alipomnunua Januari 2014 kutoka Benfica wakati yeye akiwa Meneja wa Chelsea ingawa Matic alitua kwa mara ya kwanza Chelsea Mwaka 2009 akitokea Klabu ya Serbia Kosice.
Matic alikaa Chelsea hadi 2011, akicheza Mechi 2 tu, na kisha kupelekwa kwa Mkopo huko Vitesse Arnhem, kati ya 2010 hadi 2011, na kisha kuuzwa kwa Benfica ya Ureno Mwaka 2011.

Licha kuisaidia Chelsea kutwaa Ubingwa Msimu uliopita, Kiungo huyo kutoka Serbia mwenye Miaka 28 anahisi kuwa Meneja Antonio Conte anataka kummwaga hasa baada ya kuibuka habari kuwa Chelsea inamsaka Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa France.

Nia ya Mourinho kumleta Matic Old Trafford ni kumfungua Paul Pogba awe huru kwenye idara ya Kiungo kwa kwenda mbele zaidi kuleta ubunifu kwenye Mashambulizi huku Matic akibaki Kiungo Mkabaji.

Image result for Chelsea Nemanja Matic
Mourinho pia anamlenga Kiungo Chipukizi wa Tottenham Eric Dier lakini kikwazo kikubwa ni Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, ambae ni mgumu mno kufanya nae Biashara na tayari ashatundika Dau la Pauni Milioni 50 kumn’goa Dier.