Thursday, June 22, 2017

RASMI MATAJIRI WA SINGIDA UNITED WAMSAJILI BEKI MIRAJ ADAM


Klabu ya Singida United imekamilisha mchakato wa kumsajili beki Miraj Adam ambaye alikuwa akiichezea African Lyon msimu uliopita.
Miraj ambaye aliwahi kuichezea Simba miaka ya nyuma alikuwa akiwaniwa na Singida United kwa muda na kulikuwa na mvutano kuhusu usajili wake lakini sasa rasmi amekamilisha usajili na ametua.