Wednesday, June 7, 2017

REAL YAIGOMEA OFA YA MAN UNITED KWA ALVARO MORATA

OFA ya Manchester United kumnunua Straika wa Real Madrid Alvaro Morata kwa Dau la Pauni Milioni 52.4 imekataliwa na Mabingwa hao wa Spain na Ulaya.
Kwa mujibu wa Sky Sports TV, Ofa hiyo haikumjumuisha Kipa wa Man United David de Gea ambae anatakiwa na Real.
Iliaminika Dili ni De Gea kwenda Real na Morata kutua Man United ambao pia wangeongezewa pesa juu.
Real wanataka ukimnunua Morata ulipe Pauni Milioni 78.
Morata, mwenye Umri wa Miaka 24 na ambae pia yupo Timu ya Taifa ya Spain, Msimu huu ulioisha Majuzi aliifungia Real Bao 20 na kuisaidia kubeba Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONS LIGI.
Habari toka ndani huko Old Trafford zimedai kuwa ikiwa Man United itashindwa kumpata Morata basi watamgeukia Andrea Belotti wa Torino ya Italy ambae Mkataba wake una Kipengele cha Kuuzwa kwa Dau la Pauni Milioni 87.3.
Morata ni Mzawa wa Jiji la Madrid huko Nchini Spain ambae alichipukia kwenye Vyuo vya Soka vya Real na kuibuka kuichezea Timu ya Kwanza Desemba 2010.
Julai 2014 Morata aliuzwa kwa Juventus kwa Pauni Milioni 17.5 na akiwa hapo aliisaidia Juve kutwaa Serie A mara 2, Coppa Italia 2 na pia kuifikisha Fainali ya 2015 ya UEFA CHAMPIONS LIGI walipofungwa 3-1 na Barcelona huku yeye akifunga hilo Bao 1.
Juni 2016, Real, wakitumia Kipengele cha Mkataba waliomuuza Morata kwa Juve kinachowapa uhuru wa kumnunua tena, wakailipa Juve Pauni Milioni 26.2 na kumrudisha Mchezaji huyo kwao Jijini Madrid.