Tuesday, June 13, 2017

RONALDO ASHITAKIWA LEO SPAIN UKWEPAJI KODI, MWENYEWE AWAJIBU

Real Madrid star Cristiano Ronaldo hit with tax fraud chargesWAENDESHA MASHITAKA huko Spain wamefungua Kesi wakimtuhumu Cristiano Ronaldo na Ukwepaji Kodi.
Ronaldo, Mchezaji wa Klabu ya Real Madrid humo Nchini Spain na pia ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Portugal, anadaiwa kukwepa kulipa Kodi ya Euro Milioni 14.7 kati ya Miaka 2011 na 2014.
Tangu tuhuma hizi ziibuke Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani na pia ndie Mchezaji mwenye kulipwa Pesa nyingi Duniani, amesema hana wasiwasi na uchunguzi dhidi yake kwa vile hana cha kuficha.

Imedaiwa kuwa Ronaldo alijua ‘Mfumo wa Kibiashara’ ulioanzishwa kwa makusudi ili kuficha Mapato yake yatokanayo na Haki zake za Picha na Matangazo yake.

Tuhuma zilichomoza Mwezi Desemba ilipodaiwa Ronaldo alianzisha Makampuni nje ya Spain ili kukwepa Kodi.

Alipohojiwa kuhusu uchunguzi dhidi yake na Redio ya Nchini kwao Ureno kuhusu tuhuma za Ukwepaji Kodi, Ronaldo alijibu: "Quien no debe no teme", ambayo tafsiri yake inamaanisha "Yule ambae hana cha kuficha, haogopi kitu!"

Kwa mujibu wa Magwiji wa Habari za Fedha, Forbes, Ronaldo ndie Mwanamichezo alievuna Pesa nyingi Duniani kwa Miaka Miwili mfululizo akizoa Dola Milioni 93 kutokana na Mshahara, Bonasi na Matangazo kwa Mwaka Jana.

Real Madrid star Cristiano Ronaldo hit with tax fraud chargesRichest celebrities by annual income
Sean ‘Diddy’ Combs – £102million
Beyonce Knowles – £82.7m
JK Rowling – £74.8m
Drake – £74.06m
Cristiano Ronaldo – £73.2m
The Weeknd – £72.45m
Howard Stern – £70.86m
Coldplay – £69.33m
James Patterson – £68.53m
LeBron James – £67.8m