Monday, June 19, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2017/18: DROO RAUNDI 2 ZA KWANZA MTOANO ZAFANYWA

UEFA Leo imefanya Droo ya Raundi za Mtoano ya Kwanza na ya Pili kwa ajili ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa Msimu Mpya wa 2017/18.
Kwenye Raundi ya Kwanza ya Mtoano zipo Mechi 5 na Washindi wake Watano watasonga Raundi ya Pili ya Mtoano.
Mechi za Raundi ya Kwanza ya Mtoano zitachezwa Nyumbani na Ugenini hapo Juni 27/28 na Marudiano ni Julai 4/5.
Raundi ya Pili ya Mtoano itachezwa pia Nyumbani na Ugenini hapo Julai 11/12 na Marudiano ni Julai 18/19.
Raundi hii ina Mechi 17 na Washindi wake kusonga Raundi ya 3 ya Mtoano.
Moja ya Timu kubwa ambayo ipo Raundi ya Pili ya Mtoano ni Celtic ya Scotland ambao waliwahi kuwa Klabu Bingwa Ulaya.
Ikiwa Celtic watashinda watasonga Raundi ya 3 ya Mtoano ambako watajumuika na Timu kubwa nyingine kama vile Nice na Ajax.

Droo ya Raundi ya 3 ya Mtoano itafanyika Julai 14.
Washindi wa Raundi hiyo watasonga Raundi ya Mwisho ya Mchujo ambako zitaingia Timu kama vile Liverpool, Sevilla, Napoli, Hoffenheim na Sporting Lisbon.

Droo ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo itafanywa Agosti 24.
Washindi wa Raundi hii wataingizwa Droo ya kupanga Makundi ambayo itafanywa Agosti 24.