Sunday, June 4, 2017

UEFA SUPER CUP 2017: KUPIGWA AGOSTI 8 KATI YA MABINGWA ULAYA REAL MADRID vs MAN UNITED

UEFA SUPER CUP hugombewa kila Mwaka na Washindi wa UEFA CHAMPIONS LIGI na wale wa UEFA EUROPA LIGI.
Jana Real Madrid walibeba UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kuibwaga Juventus 4-1 wakati Man United walibeba UEFA EUROPA LIGI kwa kuifunga Ajax Amsterdam 2-0.
Msimu uliopita Real walibeba UEFA SUPER CUP kwa kuitoa Sevilla kwa Bao la Beki wao Dani Carvajal kwenye Dakika za mwisho za Muda wa Nyongeza.

Manchester United to face Real Madrid in European Super CupReal walicheza Fainali hiyo kwa kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI na Sevilla walibeba UEFA EUROPA LIGI.
ITACHEZWA LINI?
UEFA SUPER itachezwa Jumanne Agosti 8.
ITACHEZWA WAPI?
Uwanja wa Fainali hii ni National Arena (Philip II Arena) Mjini Skopje Nchini Macedonia.
Ni Uwanja ambao unachukua Watazamaji 33,000 na hutumiwa na Klabu za FK Vardar na FK Rabotnički kama Uwanja wa Nyumbani.
Nchi hii inapakana na Nchi 4 ambazo bazo ni Greece, Albania, Bulgaria na Serbia.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Macedonia kuwa Mwenyeji wa Fainali kubwa ya Ulaya.
USHINDI ULIOPITA
Previous form?

Man United, chini ya Meneja Sir Alex Ferguson walitwaa UEFA SUPER Cup Mwaka 1991 walipowabwaga waliokuwa Mabingwa wa Ulaya Red Star Belgrade kwa Bao la Brian McClair.
Man United pia waligombea hili Mwaka 1999 na 2008 na kufungwa na Lazio Zenit Saint Peterburg.