Thursday, June 1, 2017

YAYA TOURE ASAINI MKATABA MPYA WA MWAKA 1 MANCHESTER CITY

KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure amesaini Mkataba Mpya wa Mwaka Mmoja.
Toure, mwenye Miaka 34, ameichezea Man City Mechi 299 na kufunga Bao 81 tangu ajiunge nao Mwaka 2010 akitokea Barcelona.
Mapema mwanzoni mwa Msimu huu uliokwisha Mwezi uliopita Toure alitemwa toka Kikosi cha City kilichosajiliwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya Meneja Pep Guardiola kukwaruzana na Wakala wa Toure, Dimitri Seluk.

Hilo pia lilimfanya Toure asipewe namba kwenye Mechi nyingine hadi pale Toure alipomwomba msamaha Guardiola mwanzoni mwa Novemba na Staa huyo toka Ivory Coast kupangwa Mechi na Crystal Palace baadae Mwezi huo na akafunga Bao 2 kwenye mechi hiyo.
Kuanzia hapo Toure akarudi Kikosini kwa kudumu na kucheza Mechi 31 akiisaidia City kumaliza Nafasi ya 3 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba huu Mpya, Toure ameeleza: “Nina bahati kuwa sehemu yah ii Klabu kubwa yenye Wachezaji wakubwa ambao wananisaidia kutimiza malengo!”

Nae Mkurugenzi wa Soka wa City Txiki Begiristain amsema: "Yaya amekuwa Mtumishi mwema kwa Manchester City na ni sehemu muhimu kwa Kikosi cha Pep Guardiola.”

Mkataba wa Toure ulikuwa umalizike Mwezi huu Juni na huu Mpya unambakiza hadi Mwakani.

Hivi karibuni City imewaacha Kipa Willy Caballero, Jesus Navas, Pablo Zabaleta, Gael Clichy na Bacary Sagna wote wakiwa wamemaliza Mikataba yao.

Tayari Wiki hii City imenunua Wachezaji Wawili Wapya ambao ni Kiungo kutoka AS Monaco Bernardo Silva waliemnunua kwa Pauni Milioni 43 na Kipa kutoka Benfica Ederson Moraes alielipiwa Pauni Milioni 35.