Sunday, July 16, 2017

ALEXIS SANCHEZ ATAKA KWENDA MAN CITY ILI ACHEZE UEFA

Arsenal star Alexis Sanchez says he has reached a decision on his futureAlexis Sanchez ameweka bayana kuwa hataki kuichezea Arsenal kwa kung’ang’ania kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI lakini ameacha uamuzi wa hatima yake kwa Arsenal.
Msimu uliopita, Arsenal walimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na hivyo kukosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI kwa Msimu Mpya wa 2017/18 na sasa watacheza UEFA EUROPA LIGI wakianzia Hatua ya Makundi.

Arsene Wenger had appeared confident that Sanchez will stay at Arsenal beyond the summerHivi sasa, Sanchez, mwenye Miaka 28, anawindwa na Manchester City na Bayern Munich wakati mazungumzo ya kuongeza Mkataba wake na Arsenal yakiwa yamekwama.
Mkataba wa sasa wa Sancheza na Arsenal unaisha Mwakani.
Wakati Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akiamini Sanchez atabakia Arsenal, Mchezaji huyo ambae kwa sasa yuko Vakesheni Mji wa Nyumbani Tocopilla Nchini Chile alinukuliwa na Redio Spoti ya Chile akisema: “Nishafanya uamuzi wangu, sasa uamuzi inabidi uchukuliwe na Arsenal!”
Aliongeza: “Ni juu yao. Inabidi nisubiri nijue wanataka nini. Kwangu mimi ni kucheza na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI. Hiyo ni ndoto yangu tangu niko Mtoto!”
Hivi sasa Arsenal wako Ziarani huko Australia lakini Sanchez alipewa Vakesheni kwa vile alikuwa na Timu ya Taifa ya Chile huko Russia kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara.

Baada ya Arsenal kuifunga Western Sydney Wanderers 3-1 hapo Jana huko Sydney, Australia, Wenger aliongea: “Ni wazi Sanchez atabaki. Hatuna vipingamizi vikubwa nae. Nimeongea nae kwa Meseji na ilikuwa safi!”

Arsenal – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]
15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]
19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup
22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)
29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)
30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)
6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)