Sunday, July 2, 2017

ARSENAL WAKARIBIA KUMBEBA LACAZETTE, KUVUNJA REKODI YAO!

Image result for Alexandre LacazetteArsenal sasa wapo karibu mno kumsaini Straika wa France Alexandre Lacazette anaechezea Klabu ya Lyon.
Mapema, Ofa ya Arsenal waligomewa wao Ofa yao kumnunua Straika huyo mwenye Miaka 26 lakini sasa inaaminika wapo karibu kukubaliwa.
Inadhaniwa Dau la Lacazette litavunja lile la Mwaka 2013 Arsenal walipoilipa Real Madrid kumnunua Mesut Ozil na kuweka Rekodi Mpya kwa Klabu hiyo.
Wakati huo Arsenal ililipa Pauni Milioni 42.4.
Mbali ya Staa huyo, Arsenal pia walikuwa Sokoni huko France lakini Ofa yao kimnunua Kiungo Thomas Lemar, mwenye Miaka 21, iligomewa.

Juzi, Mtendaji Mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis aliahidi kufanya Usajili mkubwa katika kipindi hiki.
Lakini hafi sasa Arsenal imemnunua Fulbeki wa Kushoto Sead Kolasinac akitokea Schalke ya Germany.
Lacazette, alieichezea France mara 11, alihusishwa pia na kujiunga na Atletico Madrid kabla karibuni Vigogo hao wa Spain kupigwa nyundo na CAS, Court of Arbitration for Sport, na Rufaa yao kutupwa na hivyo kutoruhusiea kusaini Mpya hadi Januari 2018.
Llacazette alichomoza Soka kuu kwa kuanza kuichezea Timu ya Kwanza ya Lyon Msimu wa 2009/10.

Tangu wakati huo amepiga Bao 129 katika Mechi 275.
Msimu uliopita alifunga Bao 28 kwenye Ligi 1 huko France akipitwa tu na Straika wa Paris St-Germain Edinson Cavani aliefunga Bao 35.
Magical Place