Sunday, July 2, 2017

CHELSEA WAMSAINI KIPA WA CITY CABALLERO NA KUTAMBULISHA JEZI MPYA YA NIKE KWA MSIMU MPYA 2017-2018.

MABINGWA wa England Chelsea wametangaza kumsaini Kipa wa zamani wa Manchester City Willy Caballero na wakati huo huo kuanua Jezi Mpya za Nike watakazotumia Msimu ujao.
Caballero, mwenye Miaka 35, anatarajiwa kuleta ushindani kwa Kipa Nambari Wani Thibaut Courtois na pia kuziba pengo la kuondoka kwa Asmir Begovic kwenda Bournemouth.
Kipa wa 3 wa Chelsea ni Kipa wa Kimataifa wa Portugal, Eduardo, mwenye Miaka 34.
Caballero alikuwa na Man City kuanzia Mwaka 2014 hadi Juzi Juni 30 Mkataba wake ulipomalizika na hivyo kuhamia Chelsea kama Mchezaji Huru.
Msimu uliopita, Caballero, Raia wa Argentina, aliichezea Man City Mechi 26.
Kabla kujiunga na City, Caballero alicheza na Malaga na Elche huko Spain na kabla ya hapo aliidakia Boca Juniors Nchini kwao Argentina.

WAKATI huo huo, Chelsea imeanua Jezi Mpya zilizotengenezwa na Kampuni ya Nike kwa ajili ya Msimu Mpya wa 2017/18 wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, ambao wao ndio Mabingwa Watetezi.

Hii itakuwa kwa mara ya kwanza katika Historia ya Chelsea kuvaa Jezi za Nike.
Wakati Jezi za Mechi za Nyumbani ni za Kibuluu zile za Mechi za Ugenini ni Nyeupe.

Will Chelsea have a Premier League title to defend next season?