Wednesday, July 12, 2017

ERIC DIER WA SPURS AJISOGEZA KWA JOSE MOURINHO.

KIUNGO Eric Dier ameishitua Klabu yake Tottenham Hotspur kwa kuwapasulia kuwa anataka kujiunga na Manchester United ili afanye kazi na Jose Mourinho.
Baada ya kumkosa Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic kwa sababu ya 'kuwapora' Romelu Lukaku, sasa Man United wapo njiani kuwasilisha Ofa ya Dau la Pauni Milioni 40 kumnunua Dier.
Lakini Dau hilo lipo chini ya Pauni Milioni 60 ambazo Spurs ndizo wanazoona ndio thamani halisi ya Eric Dier mwenye Miaka 23.
Hata hivyo, Man United wanaamini watafikia muafaka na Spurs ingawa wanamhofu Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ambae ni mgumu mno kufanya nae biashara.

Hilo lilionekana wakati Man United walipowanunua kutoka Spurs Michael Carrick Mwaka 2006 na Dimitar Berbatov Mwaka 2008 na dili hizo kukamilishwa kwa mbinde na kwa bei ghali mno.
Lakini safari hii presha ya Mchezaji mwenyewe Dier kutaka kuhama huenda ikawasaidia mno Man United.
Tayari Dier ameshawaambia Maswahiba wa karibu yake kuwa anafurahia kufanya kazi na Mourinho.
Pia, mvuto mkubwa kwake Dier kwenda Man United ni kuongezeka mno kwa Mshahara wake kutoka Pauni 70,000 anazopata sasa huko Spurs na kupanda hadi zaidi ya Pauni 150,000 atakazopata akijiunga na Man United.