Monday, July 3, 2017

EVERTON WAMSAINI SANDRO WA MALAGA

Straika wa Malaga, Sandro Ramirez, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Everton.
Msimu uliopita Chipukizi huyo wa Miaka 21 alifungia Malaga Bao 14 baada ya kujiunga nao kutoka Barcelona.
Everton wanatarajiwa kumasaini Beki wae, kwa Dau la Pauni Milioni 24.
Tayari Everton wameshawasaini Kipa wa England U-21 kutoka Sunderland,Jordan Pickford, kwa Pauni Milioni 30 na Kepteni wa Ajax ya Netherlands, Davy Klaasen, kwa Pauni Milioni 24.